MSAJILI wa Hazina nchini, Lawrence Mafuru amesema benki nchini
zinashindwa kueleza ukweli juu ya kuyumba kwao na kwamba madai ya kuwa
hali zao ni mbaya kutokana na agizo la serikali la kutaka fedha zake
zitunzwe Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hazina ukweli.
Mafuru amesema taarifa ambazo serikali wanazo ni kwamba benki hizo
zaidi ya 50 zimekopesha fedha nyingi kwa watu mbalimbali, lakini
marejesho ya madeni hayo yamekwama kiasi cha kusababisha benki hizo ziwe
katika hali hiyo.
Akizungumza jana Dar es Salaam, Msajili wa Hazina licha ya kukiri
kuwa mzunguko wa fedha umepungua kutokana na Tanzania kuchagua kwamba
fedha inazozipata zitumike katika miradi ya maendeleo badala ya matumizi
ya kawaida, benki zinazolalamika zimeshindwa kurejesha fedha
ilizokopesha watu na taasisi mbalimbali.
Akizungumzia taarifa zinazoenezwa kwamba benki zimekosa fedha za
kujiendesha, Mafuru alisema taarifa walizozipata ni kwamba Septemba
mwaka huu, benki hizo zaidi ya 50 nchini zimekopesha zaidi ya Sh
trilioni 16.3 kwa watu mbalimbali.
Hata hivyo, alisema kati ya fedha hizo, Sh trilioni 1.43 zimekopeshwa
bila ya kurudishwa katika benki husika na kwamba benki hizo zinashindwa
kueleza ukweli uliopo badala yake wanalalamika kwamba hatua ya serikali
kuamua fedha zake zitunzwe BoT badala ya katika benki za kibiashara,
ndio sababu ya hali yao (benki) mbaya.
Kwa mujibu wa Mafuru, serikali imeamua kuchukua uamuzi huo wa kuzitoa
fedha zake kutoka katika benki mbalimbali za kibiashara nchini kwa
ajili ya kuwezesha serikali kujua mapato wanayopata kutoka katika
taasisi zake.
Msajili wa Hazina amesema zaidi ya Sh bilioni 515 zimeingizwa BoT
baada ya uamuzi huo wa Serikali ya Awamu ya Tano ambao ulitangazwa na
Rais John Magufuli baada ya kushika madaraka mwaka mmoja sasa.
Mafuru
alikiri kuwa ni kweli kwamba mzunguko wa fedha umekuwa mdogo na kueleza
kuwa chanzo chake si kwamba benki zimekosa fedha kwa ajili ya
kujiendesha.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: