ads

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli tayari amekwishasaini mabadiliko ya sheria yanayomtaka mwajiri kukata asilimia 15 ya mshahara wa mwajiriwa ambaye ni mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu kwa ajili ya kulipa deni lake analodaiwa na Bodi ya Mikopo.


Taarifa hiyo imetolewa  na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Mhandisi Stella Manyanya, ambapo amesema kuwa makato kiwango hicho kimepanda kutoka asilimia 8 ya sasa.

"Hii asilimia 15, kimsingi sheria ninavyofahamu ilishasainiwa, baada ya hapo kuna kuiangalia iendane na kanuni zetu, baada ya kuicheki imeendana na kanuni zetu kama kuna sehemu itahitaji kuboreshwa kidogo haitazidi miezi miwili au mitatu, baada ya hapo tutaweza kutumia hiyo 15%, na asilimia 15 ya safari hii ni tofauti na siku za nyuma, siku za nyuma tulikuwa tunachaji asilimia 8”, amesema Manyanya. 

Hapo awali wadaiwa hao wa mikopo walikuwa wanakatwa asilimia 8, lakini sheria ya sasa itaruhusu wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kukatwa asilimia 15 ya kipato chao.

Pia Manyanya amesisitiza kuwa kwa wale ambao hawajaajiriiwa, lakini wanafanya biashara zao wanatakiwa kuwasilisha angalau shilingi 120,000 kila mwezi na kuwashauri kuwa ni vema wakapeleka zaidi ili wamalize haraka madeni yao.

Kuhusu wasio na kazi, amesema haiwezekani mtu asome halafu akose shughuli ya kufanya na kuwataka kutafuta shughuli yoyote ya kufanya ili waanze mapema kulipa madeni yao ndani ya miaka miwili baada ya kuhitimu  masomo.
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: