![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa jana aliongoza mamia ya waombolezaji
kumuaga baba mzazi wa Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda, Mzee Xavery
Mizengo Pinda (90) huku Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete
akimuelezea mzee huyo kwamba alikuwa mtu mkarimu na Mcha Mungu.
Shughuli za kuaga mwili wa marehemu zilifanyika nyumbani kwa Waziri
Mkuu mstaafu Pinda kwenye Kijiji cha Zuzu mjini hapa na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali wakiwamo mawaziri, naibu mawaziri, wabunge, viongozi
wa chama na serikali, viongozi wa dini na wananchi.
Waziri Mkuu Majaliwa alisema serikali itaratibu shughuli zote na
itawakilishwa kwenye maziko na Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge
wa Mlele, Isaack Kamwelwe.
“Niliwahi kufika hospitalini kumuangalia kwa kweli hali yake haikuwa
nzuri, tumuombee apumzike kwa amani,” alieleza Kikwete na kuongeza kuwa
wakati akiwa Rais alifanya ziara Mkoa wa Katavi na alipita Kijiji cha
Kibaoni kumsalimia mzee huyo. “Alikuwa ni mtu mwema na mwenye upendo
mkubwa, alikuwa akitambua ugumu wa kazi za uongozi wa taifa alituombea.
Alisema uongozi ni kuvumilia na kupokezana kijiti,” aliongeza Rais
mstaafu Kikwete akimkariri Mzee Pinda.
Alisema Pinda alimpa taarifa za kifo cha baba yake na kufika ili
kumuaga marehemu. Waziri Mkuu mstaafu Pinda akizungumza alisema
kuondokewa na baba si jambo rahisi, lakini anamshukuru Mungu kwa kila
jambo.
“Siku za mwisho za uhai wake zilikuwa nzuri, lakini mimi nilijua
haiwezekani tena.” Akiongoza ibada nyumbani hapo, Padri Chesco Msaga wa
Kanisa Katoliki alisema kila mwanadamu anatakiwa kuishi maisha ya
kumpendeza Mungu, wakati Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa alisema Mzee Pinda alitumia
uhai wake vizuri na aliyoyaacha yaendelee kuokoa walio wengi.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: