![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
MBUNGE wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema),
alikamatwa na polisi jijini Dar es Salaam akituhumiwa kuingilia
utekelezaji wa majukumu ya jeshi hilo jana.
Waitara alikamatwa eneo la Uvikiuta alipokuwa akifuatilia mgogoro wa
muda mrefu wa ardhi na kupelekwa kwenye Kituo cha Polisi Chang'ombe,
Temeke jijini.
Waitara alidai hakuzuia jeshi
hilo kutekeleza majukumu yake isipokuwa alihoji sababu za nyumba za
wananchi wa Mtaa wa Uvikiuta uliopo Kata ya Ukonga kuvunjwa pasi na
taarifa, na kampuni moja ya udalali chini ya jeshi hilo.
Alisema jana majira ya saa mbili asubuhi alipata taarifa za wananchi
wake kuvamiwa na watu wanaojita kampuni ya madalali ambao walifika
katika eneo lao na kuanza kuvunja nyumba na alipoamua kuhoji sababu za
zoezi hilo kufanywa bila taarifa, alikamtwa na kupelekwa polisi kwa
madai kwamba amezuia jeshi kutekeleza majukumu yao.
“Mimi sijazuia jeshi kufanya kazi yake, nilikuwa nahoji tu kwa nini
iweje ghafla hivyo na ninavyofahamu mgogoro huo ulikuwa wa siku nyingi
na kesi yake bado iko mahakamani," alisema Waitara. "Sasa kwa nini waje
kuvunja wakati kesi inaendelea na hata hivyo wananchi hawajapewa
taarifa?”
Alisema kuwa jana mchana alipewa fomu ya kuandika maelezo yake,
lakini akaomba a
siandike chochote mpaka awasiliane na Mwanasheria wake.
“Tangu saa nne asubuhi nilikuwa nahojiwa polisi hadi saa 12 jioni
ndiyo nimetolewa. Wanadai nimezuia polisi kutekeleza majukumu yao,
wamekubali kuniachia kwa dhamana lakini wameniambia niende kesho saa
mbili asubuhi kwa RCO," alisema Waitara jana.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: