KOCHA wa Simba Joseph Omog, ametishia kumkata mshahara mchezaji
yeyote atakayechelewa kuripoti kwenye mazoezi ya timu hiyo kwa ajili ya
kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ambao
umepangwa kuanza Desemba 17 mwaka huu.
Simba ndiyo vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 35, wamepanga kuanza
mazoezi leo Jumatatu, kujiandaa na ligi hiyo ambayo imeonesha kuwa na
ushindani mkubwa msimu huu.
Akizungumza jana Omog, raia wa Cameroon, alisema
amezungumza na wachezaji wote wakati akiagana nao kwenda kwenye
mapumziko hayo mafupi hivyo hatokuwa na msamaha kwa yeyote ambaye
atachelewa kufika mazoezini pasipo sababu za msingi.
“Simba ni timu kubwa na ina malengo yake iliyojiwekea malengo yetu
msimu huu ni ubingwa na ili tuchukue ubingwa lazima tufanye kila kitu
kwa pamoja na kwa wakati haiwezekani wengine waje siku ya kwanza wengine
wachelewe wote ni kitu kimoja ndiyo maana nimesisitiza kukata mshahara
kwa kila atakayechelewa,”alisema Omog.
Kocha huyo alisema wachezaji wote wa Simba ni profeshno, wanatambua
majukumu yao na mikataba yao inavyoelekeza hivyo haoni sababu ya
kupigizana kilele kwa sababu kila mtu anatambua wajibu wake kutokana na
kanuni za klabu zinavyoelekeza.
Alisema kwa kutambua hilo ndiyo maana yeye kama kiongozi mkuu tayari,
amewasili kwenye kituo cha kazi tayari kwa maandalizi hayo ambayo
wanalazimika kuyafanya kwa umakini ili kutimiza kile ambacho wamekusudia
kukifanya msimu huu nacho ni ubingwa.
“Ligi imekuwa ngumu na yenye ushindani hivyo bila kujipanga mapema
tunaweza kupoteza nafasi yetu ya kuongoza ligi ifahamike kwamba tupo
mbele kwa tofauti ya pointi mbili kati yetu na Yanga, kwa hiyo ni lazima
tufanye jitihada kwa kuongeza bidii ya kupambana ili kupate kile
tunachokihitaji,” alisema Omog.
Simba inalazimika kupambana kufa au kupona ili kutwaa ubingwa msimu
huu baada ya kupita katika kipindi kigumu cha misimu mitatu bila kutwaa
taji lolote katika michuano yote iliyoshiriki ndani ya nchi.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: