![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Katibu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif amelishutumu jeshi la
polisi kwa kile alichodai kuvuruga mikutano inayoandaliwa na wafuasi wa
chama hicho wanaomuunga mkono katibu mkuu huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amedai
kushangazwa na nguvu kubwa inayotumiwa na polisi katika kuzuia mikutano
ya ndani inayoandaliwa na wafuasi wa chama hicho wanaomuunga mkono huku
wakiruhusu inayoandaliwa na mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim
Lipumba.
“Mpaka muda ninavyoongea na nyinyi waandishi wa habari gari iliyokuwa
kituoni kama kielelezo au sahihi limeondolewa kituoni hapo na
watuhumiwa wote wameachiwa huru na wapo mitaani huku wakitamba
wanalindwa na jeshi la polisi. Wamekuwa wakitisha katika mitandao ya
kijamii na katika mazingira ambapo wapo wanachama wa CUF bila ya hofu
kwani wanaamini na kusema waziwazi kwamba jeshi la polisi ni sehemu yao
na haliwafanyi lolote,” alisema Seif.
Aidha Maalif Seif alisema kuwa suala la kuachiwa huru watuhumiwa wa
utekaji nyara wa viongozi na wanachama wa CUF ni ukiukaji wa haki na
kumtaka waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba kuingilia kati.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: