![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Wachezaji saba
walikosekana wakati kocha mpya wa Yanga, George Lwandamina akishudia kwa
mara ya kwanza mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika jana asubuhi kwenye
Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini, Dar es Salaam.
Katika
mazoezi hayo ya jana yaliyodumu kwa saa mbili, wachezaji waliokosa ni
kipa, Benno Kakolanya, mabeki Hassan Kessy, Vincent Bossou, kiungo
Haruna Niyonzima na washambuliaji Donald Ngoma, Malimi Busungu na Obrey
Chirwa.
Hata
hivyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit alisema kuwa wachezaji
ambao hawakuonekana mazoezini, wana ruhusa maalumu ya uongozi.
Mabingwa
hao watetezi wa Ligi Kuu wameanza mazoezi kujiandaa na mzunguko wa pili
wa Ligi Kuu utakaoanza Desemba 17. Yanga itaanza raundi ya pili kwa
kupambana na JKT Ruvu.
Katika
mazoezi hayo, Lwandamina alikuwa nje na mkurugenzi mpya wa ufundi wa
Yanga, Hans Pluijm na kumwachia jukumu kocha msaidizi, Juma Mwambusi
kuwanoa wachezaji.
Lwandamina
alionekana akiandika vitu mbalimbali katika kile alichokuwa akikiona
katika mazoezi hayo na baada ya mazoezi aliliambia gazeti hili kuwa kazi
yake kubwa katika mazoezi hayo ya kwanza ni kufuatilia ubora wa
wachezaji wake.
“Nilikuwa
ninaangalia ubora wa wachezaji, lakini kazi rasmi nitaanza kesho (leo)
na nimeridhishwa na ubora wa wachezaji nafikiri kidogo nimeanza kupata
mwanga wa wapi pa kuanzia,” alisema Lwandamina.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: