![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
SIKU moja baada ya kuanza kibarua chake kipya cha kuinoa klabu ya
Yanga, kocha mpya wa mabingwa hao wa soka nchini, George Lwandamina
ameonesha kutoridhishwa na ubora wa uwanja unaotumiwa kwa mazoezi wa
Chuo cha Polisi Kurasini na kuutaka uongozi kutafuta uwanja mwingine.
Mzambia huyo alianza rasmi kibarua chake Jumatatu, ambapo baada ya
kumalizika kwa mazoezi yaliyohudhuriwa na wachezaji 18, aliuomba uongozi
kumuonesha viwanja vingine vitatu tofauti ili kuchagua ulio bora
tofauti na huo wa Polisi Kurasini.
“Uwanja huu ni mzuri kwa utulivu, lakini una mapungufu mengi ikiwemo
sehemu ya kuchezea kukosa usawa, jambo ambalo linasababisha mpira
kudunda dunda na kumpa tabu mchezaji kuumiliki,”alisema Lwandamina.
Kocha huyo alisema anaamini Tanzania kuna viwanja vingi vizuri
ukiacha ule wa Taifa, ambao umefungiwa kwa sasa kwa timu hizo za Simba
na Yanga, hivyo viongozi watapambana ili kuwatafutia uwanja mzuri ambao
utamwezesha yeye na wasaidizi wake kutoa mafunzo mazuri kwa wachezaji
wao.
Akilizungumzia hilo, Meneja wa timu hiyo, Hafidh Salehe alisema
watalifanyia kazi ombi la kocha huyo na muda si mrefu watalipatia
ufumbuzi ili timu hiyo ihamishie mazoezi yake kwa ajili ya kujiandaa na
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.
Siku za nyuma Yanga ilikuwa ikipendelea kufanya mazoezi yake kwenye
viwanja vitatu ule wa Uhuru, Gymkhana au Boko Veterani na kutokana na
maombi ya Lwandamina pengine uongozi ukapendekeza timu kufanya mazoezi
yake moja kati ya viwanja hivyo.
Hata hivyo, Tanzania imekuwa na matatizo makubwa ya viwanja huku
klabu kongwe za Yanga na Simba zikiwa hazina viwanja vyao na kubaki
kukodisha.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: