![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema katika hesabu za Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali za mwaka 2014/2015, zimeonesha kwamba,
limepata faida ghafi ya Sh bilioni 186 na ya uendeshaji ya Sh bilioni
263.
Faida hiyo iliyopatikana kwa mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu,
inatokana na shirika hilo kuwa katika hali nzuri, baada ya kuwa limetoka
katika kupata hasara ghafi ya Sh bilioni 496 kwa mwaka 2013, huku
upotevu wa umeme ukipungua kutoka asilimia 21 mwaka 2012 hadi asilimia
17 mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Felchesmi Mramba amesema hayo hivi
karibuni kuwa rasilimali zake zimeongezeka kutoka Sh trilioni 3.8 mwaka
2013 hadi trilioni 5.2 mwaka 2014 ikiwa ni ongezeko la asilimia 36.8.
Alisema si kweli kuwa sekta ya umeme ina hali mbaya kwani ni nzuri na
yenye maendeleo kwani kipindi kama hiki mwaka jana kulikuwa na upungufu
wa megawati 300 za umeme na kulikuwa na mgawo lakini sasa hakuna
upungufu wa umeme wakati mahitaji yakiongezeka kutoka megawati 1000 kwa
wakati huo hadi 1041.
Mramba amesema kuhusu matatizo ya bili za wateja kwa kutumia mfumo wa
luku tayari asilimia 96 ya wateja wote nchini wanatumia mita hizo hivyo
kuondoa malalamiko ya bili na asilimia nne iliyobaki iliyo katika mikoa
ya Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Mwanza itakuwa imebadilishwa kuwa na
luku ifikapo Machi, mwakani.
Amesema nchi itakuwa ya kwanza kwa wateja wake wote kutumia mita za
luku huku mfumo wake umeboreshwa na tayari asilimia 41 ya kukatika
katika kwa umeme imeondolewa na wanatarajia ifikapo Februari mwakani,
utakuwa ukikatika kwa nadra.
Kuhusu kupandishwa kwa bei ya umeme, Mramba amesema imepeleka
mapendekezo kwa mdhibiti kama sheria inavyowataka ili bei iangaliwe na
gharama halisi, bei waliyoomba haitawaathiri wateja wadogo wa kawaida
bali makundi ya kibiashara.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: