![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Katibu Mkuu wa
Chadema, Dk Vincent Mashinji ameizungumzia operesheni Umoja wa Kupinga
Udikteta Tanzania (ukuta) ambayo ilifanyiwa figisu kadhaa wakati wa
utekelezaji wake hadi chama hicho kikaamua kuiweka kando kwa muda.
Dk Mashinji amesema mikutano na maandamano ilikuwa moja ya mikakati ya kufanikisha Ukuta.
“Sisi
tulipotangaza Ukuta, tulitangaza mchakato kwa kuunda kamati ambazo ni
pamoja na ya mawasiliano kueleza Ukuta ni nini; kamati inayowasiliana na
wadau wa nje kama vile vyama vya wafanyakazi, wadau wa nje ya nchi;
kamati iliyokuwa ikiratibu matukio ambayo sasa ndiyo hiyo waliyotegemea
maandamano na mikutano,” amesema.
“Kuna
kamati iliyokuwa ikihusika na mashauriano ya mikakati vikiwemo vyombo
vya habari na kamati ya sheria.Unapopinga kitu chochote unapitisha
ujumbe kwa wananchi ili wapate maana ya Ukuta.”
“Kwa
hiyo Ukuta ni mwenendo wa maisha na ni endelevu siyo wa kuishia
Septemba 1, ilikuwa ni kujipanga tu. Tulitumia neno ‘defiance’ ambalo
wenzetu walilitafsiri kama uhaini, kitu ambacho siyo sawa,” amefafanua.
“Kwanza
tulifanikiwa kupeleka tafsiri kwa watu. Wengi sasa wameshaelewa
udikteta ni nini. Watu wanadhani demokrasia ni kufanya uchaguzi tu,
demokrasia ni pana, uchaguzi ni sehemu tu. Ni pamoja na kusikilizwa,
pamoja na kutoingiliwa uhuru wa mtu binafsi, ndiyo maana sisi tunasema
Ukuta ulifanikiwa sana,” amesema Dk Mashinji.
Akizungumzia
sababu za kuahirishwa kwa utekelezwaji wa Ukuta, Dk Mashinji amesema
kulikuwa na sababu za msingi ikiwa pamoja na kuwaheshimu viongozi wa
dini waliokuwa wakitafuta suluhu.
“Sasa
kama viongozi wa dini wanasema, hili jambo mnalofanya ni zuri na sisi
tumeliona, tunaomba tukamweleze bwana mkubwa nini kinaendelea. Sasa
swali linakuja, kama wewe umesimama kwenye viatu vyetu, utaendelea au
utaacha? Sisi kwa busara ya kawaida tuliona tuwasikilize,” amesema.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: