![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
RAIS mstaafu wa awamu ya tatu ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM), Benjamini Mkapa, amewataka viongozi wa vyuo vikuu nchi
nzima kukutana kwa lengo la kujadili gharama za uendeshaji wa vyuo hivyo
nchini.
Ametoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya saba ya chuo hicho na
kufafanua, “Jambo hilo lisipozungumzwa sasa linaweza kuwa tatizo kubwa
siku za usoni”.
Amesema nchi bado changa lakini kwa sababu uchumi wa nchi ni mchanga
kwa maana hiyo bado ni nchi masikini, hivyo wanajitahidi kukuza uchumi
kwa kasi lakini matarajio na idadi ya wanachuo na wanafunzi ni kubwa na
inazidi kukua siku hadi siku.
Amesema kukua huko ni lazima kufanane na uwezeshaji wa vyuo vyote
kutoa elimu na kama bajeti hazitoshelezi yatapatikana matokeo hafifu na
ushindani katika jumuiya ya Afrika Mashariki, Afrika na dunia nzima na
kwa wahitimu hapa nchini utakuwa mgumu sana.
Mkapa amesema amri na maagizo peke yake hayatatui tatizo ila viongozi
wakikaa pamoja wanaweza kujadili mikakati ya kugharamia jambo ambalo
linanza kuimarisha ubora wa elimu na umakini wa rasilimali watu
wanaotokana na vyuo vikuu vya serikali.
Amesema chuo cha UDOM kutegemea uwekezaji wakati chenyewe kinawekezwa
ni kujidanganya, hivyo wakiamua kufanya mkutano wanaweza kupata
ufumbuzi katika vyuo hivyo.
Mwenyekiti wa chuo kikuu cha UDOM, Gaudencia Kabaka katika risala
yake alisema changamoto kubwa waliyonayo chuoni hapo ni kutolipwa kwa
wakati fedha za ada na bodi ya mikopo.
Ameisema kuwa mwaka 2015/2016 ada ya Sh bilioni 6.5 ambazo zilitakiwa
kulipwa na bodi ya mikopo hazijalipwa mpaka sasa. Jumla ya wanafunzi
4,839 walihitibu,kati ya wahitimu hao waliopata cheti ni 394, stashahada
4,046, shahada ya kwanza 242, stastahada za juu 62 na shahada za
uzamili na 17 shahada za uzamivu.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: