Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Waziri wa Katiba na
Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe kumpa maelezo kuhusu sababu za Tanzania
kutokukamilisha mkataba wa Mawakili wa Afrika Mashariki kutambuana
katika utendaji wao.
Ametoa agizo hilo leo wakati akimuwakilisha Rais Dk. John Magufuli
katika ufunguzi wa mkutano wa 21 wa mwaka wa Chama cha Wanasheria wa
Afrika Mashariki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
“Nimeshtushwa kidogo kusikia kwenye taarifa yenu kuwa mkataba huo
uliolenga nchi zote za Afrika Mashariki hautaihusisha Tanzania kutokana
na kutokukamilisha sehemu yao ya kuufanyia kazi, nitahitaji maelezo,”
“Nitapenda kupata maoni yako wewe mwenyewe Mheshimiwa Waziri wa
Katiba na Sheria wa Tanzania kwa vile wewe ni Mwanasheria mwandamizi na
siyo Mwanasheria wa Tanganyika Law Society peke yake kwa nini Tanzania haijakamilisha mkataba huu,” amesisitiza.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: