ads

KOCHA mpya wa Yanga, George Lwandamina, jana aliripoti kwa mara ya kwanza makao makuu ya klabu hiyo na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa timu hiyo, Baraka Deusdetit.


Katika mazungumzo hayo, walipanga siku ya kuanza rasmi kazi pamoja na mipango mingine ya timu hiyo kuelekea kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu.

Mmoja wa viongozi wa klabu hiyo ambaye alikuwapo klabuni hapo wakati wa kuwasili kwa kocha huyo majira ya saa 9:05 mchana, alisema Lwandamina alitumia zaidi ya saa moja kufanya mazungumzo na Baraka kabla ya kutembezwa kwenye ofisi nyingine za klabu hiyo na kuangalia mazingira ya makao makuu hayo ya klabu.

"Kocha alionekana mwenye furaha muda wote, alitembezwa kila eneo na kupewa maelekezo na hii ni ishara sasa ameanza kazi rasmi kwenye klabu yetu," alisema kiongozi huyo.

Kwa upande wake, Baraka hakutaka kuzungumza lolote huku akiahidi kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuelezea mikakati ya klabu hiyo kuelekea kwenye mzunguko wa pili wa ligi kuu uliopangwa kuanza Desemba 17.

Imeelezwa kocha huyo leo atakutana na wachezaji wake kwa mazungumzo kabla ya kuanza rasmi mazoezi kesho jioni jijini Dar es Salaam.

Lwandamina alisaini mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha Yanga akichukua nafasi ya kocha Hans van der Pluijm ambaye kwa sasa anakuwa Mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo.

kabla ya kujiunga na Yanga, Lwandamina alikuwa kocha mkuu wa Zesco ya Zambia na aliifikisha kwenye hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Afrika msimu uliopita

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
 
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: