![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Baada ya kuikanyaga Spurs kwa mabao mawili kwa moja, meneja wa vinara
wa ligi ya nchini England (chelsea) Antonio Conte, amewataka mashabiki
kuendelea kumpa ushirikiano katika kipindi hiki cha kuelekea mpambano
dhidi ya Man city.
Kikosi cha Chelsea kitasafiri hadi Etihad Stadium mwishoni mwa juma
hili, kwa lengo la kuzisaka point tatu muhimu mbele ya Pep Guardiola.
Conte amesema mchezo huo utabeba umuhimu mkubwa kwa Chelsea kutokana
na umahiri wa kikosi cha wapinzani wao, na anaamini huenda kikawa kipimo
tosha kwa wachezaji wa The Blues kwa msimu huu.
Amesema mtihani huo unapaswa kupewa ushirikiano na mashabiki wa
Chelsea kwa kuishangilia timu yao ambayo kwa sasa ipo kileleni kwa
kufikisha point 31.
“Ni muhimu kwa kila shabiki kutuunga mkono, kutokana na uzito wa
mchezo utakaotukabili mwishoni mwa juma hili, ninatarajia kuwaona
wakishangilia wakati wote tutakapokua Etihad Stadium,” Alisema Conte.
“Tunapokua Stamford Bridge mashabiki wetu hujivunia kuwa nyumbani,
lakini bado wana nafasi ya kuwa nasi hata katika uwanja wa ugenini na
tukaonekana tupo nyumbani pia.
“City ni timu nzuri na wanajua nini wanachokihitaji ndani ya dakika
90, lakini juhudi zetu za kuwakabili hazitotosha kama mashabiki
hawatokua pamoja nasi,” Alionega meneja huyo kutoka nchini Italia.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: