![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
UZALISHAJI katika kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara
umesimama kwa muda kutokana na hitilafu za kiufundi zilizojitokeza
katika mitambo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dangote Tanzania, Harpreet Duggal alisema jana
kwamba mafundi wa Dangote wapo kazini na shughuli za uzalishaji
zitarejea katika siku chache zijazo.
Alisema kiwanda kinachomilikiwa na bilionea namba moja Afrika, Alhaji
Aliko Dangote wa Nigeria kilianza uzalishaji wa kibiashara mwaka huu na
kama ilivyo kwa kiwanda kingine kama hicho, jambo lolote linaweza
kutarajiwa hasa katika miezi ya mwanzo.
Alisisitiza, “hitilafu hizi ni za kawaida na uzalishaji utarejea katika kipindi kifupi kijacho.”
Akizungumzia gharama za uzalishaji, Duggal alisema uendeshaji nchini
uko juu huku miongoni mwa sababu ikiwa ni matumizi ya jenereta za dizeli
katika kuendesha kiwanda.
Hata hivyo, alisema serikali inaangalia suala hili la gharama na jinsi ya kutafuta njia ya kuwapunguzia mzigo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: