Serikali ya Zambia
imewataka watendaji wake na wale wa Tanzania kuchapa kazi na kuacha
kupiga soga ili kuinua uchumi wa nchi hizo.
Rais
wa nchi hiyo, Edgar Lungu amesema hayo wakati wa kuhitimisha ziara yake
ya siku tatu baada ya kutembelea Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na
Shirika la Kusafirisha na Kupokea Mizigo la Zambia (Zamcargo).
Amesema
licha ya kuenzi mchango wa waasisi wa mataifa hayo, Mwalimu Julius
Nyerere na Kenneth Kaunda, watajikita zaidi kwenye biashara.
“Changamoto
mliyonayo ni kwenu uongozi na Bodi ya TPA kwa watu wa Kusini au
Mashariki au hata nje ya Afrika. Watu wa Zambia wanasema muda wa siasa
umekwisha, sasa ni muda wa maendeleo. Hatutawaunga mkono kwa sababu niko
karibu sana na Rais (John) Magufuli. Ni kweli niko karibu na Rais
Magufuli kama mlikuwa hamjui, lakini hatuwaungi mkono kwa sababu hiyo,
bali kwa ufanisi wenu,” amesema Rais Lungu.
Akizungumzia miradi ya reli ya Tazara na bomba la mafuta la Tazama, Rais Lungu amesema nayo inapaswa kufanya kazi kwa ufanisi.
“Ni
kweli sisi ni ndugu lakini hatuangalii hilo. Wazambia wanataka mbolea
ifike haraka, shaba isafirishwe haraka kwenda sokoni,” amesema.
Awali,
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko amesema mwaka 2014, Zambia
ilichangia asilimia 36 ya mizigo ambayo ni sawa na tani milioni 5.2
ikiwa ni mbali ya nchi nane zinazotumia bandari hiyo.
“Kwa
mfano muda wa kutoa mizigo bandarini umepunguzwa hadi siku kumi na moja
mwisho wa Oktoba kulinganisha na siku 32 zilizokuwa mwaka 2008. Bandari
pia imeboresha mfumo wa malipo ya mizigo kwa wateja wake kwa kutumia
mfumo wa kielektroniki,” amesema Kakoko.
Mara
baada ya ziara hiyo, Rais Magufuli amewaongoza viongozi wengine wa
Serikali kumsindikiza mgeni wake huyo uwanja wa ndege na kurejea Zambia.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: