Matokeo ya Uchaguzi
Mkuu wa mwaka jana bado yanaiumiza Chadema ambayo imesema haitakubali
yaliyotokea yajirudie katika uchaguzi ujao.
Katika
uchaguzi huo, chama hicho kilishika nafasi ya pili nyuma ya CCM lakini
kililalamikia matokeo huku kikisema kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na
sheria za uchaguzi.
Rais
John Magufuli alishinda uchaguzi huo kwa kupata kura 8,882,935, huku
mpinzani wake, Edward Lowassa wa Chadema akipata kura 6,072,848.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema chama hicho hakitakubali kudhulumiwa kwa namna yoyote ile ushindi.
“Hii
inaonyesha katika nchi yetu bado kuna tatizo la utendaji haki. Wewe
umefanya mara ya kwanza, tukanyamaza, ukafanya tena mara ya pili tena
kwa ubabe, tukalalamika, badala ya kusema njooni tuongee, unasema
nendeni kokote. Sawa, tusubiri awamu ya tatu. Tukishindwa tutakupongeza,
lakini tukishinda shughuli yake itakuwa ngumu,” amesema.
Kuhusu
utawala wa Rais Magufuli, Dk Mashinji amesema kumekuwa na ukiukwaji wa
utawala bora na matokeo yake yeye ndiyo amekuwa kila kitu.
“Wakati anaanza mapambano dhidi ya rushwa tuliamini angeweza kuliondosha tatizo hili, lakini hali ikawa tofauti,” amesema.
Amesema kadri siku zinavyokwenda, Serikali imeshindwa mapambano dhidi ya rushwa.
Pia,
amesema katika mwaka mmoja huo wa Magufuli ameshindwa kusimamia
utawala bora baada ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara na shughuli
zote za siasa nchini kwa kile alichosema kuwa muda wa siasa umekwisha.
“Tuliposema
hivi, watu wengi hawakutuelewa, lakini wakati anatuzuia tusifanye
siasa, watu wengi walisema wale wanasiasa wamezidi,” amesema.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: