![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Mchungaji wa Kanisa
la Maombezi, Anthony Lusekelo ametoa ya moyoni kuhusiana na wanasiasa
Kingunge Ngombare Mwiru na Edward Lowassa akitaka waombwe radhi.
Lusekelo
maarufu kwa jina la Mzee wa Upako amesema wanasiasa hao wamekosewa na
Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho amekitaka kiwapigie magoti Watanzania
hao.
Mchungaji
huyo amesema hayo katika mahojiano maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake
Kawe jijini Dar es Salaam ametumia muda mwingi kueleza jinsi Lowassa na
Kingunge walivyo muhimu kwa CCM.
Lowassa,
ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, na
Kingunge ambaye ni mwanasiasa mkongwe aliyefanya kazi kwa karibu na
awamu zote nne za kwanza, walihama CCM wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu
mwaka jana, wakipinga uendeshaji mchakato wa kupata mgombea urais kwa
tiketi ya chama hicho.
“Unawezaje
kumuacha Mzee Kingunge na Lowassa wakaenda kwenye vyama vingine? Wale
ni asset (mali). Ingekuwa mimi, ningerudi na kumpigia magoti Mzee
Kingunge na kumwambia ‘Mzee chama kinakuhitaji rudi tukijenge,” amesema.
Mchungaji huyo maarufu amesema CCM imetumia muda mrefu kuwafinyanga viongozi hao, kwa hiyo ni hasara kwa chama kuwaacha.
“Mimi
ninachojua ni kuwa Lowassa ni kiongozi mzuri, ana ubinadamu. Katika
watu ambao Mungu alitujalia kuwa viongozi, Lowassa yumo. Hata uniambie
Lowassa mwizi, mimi sikubali,”amesema.
Lusekelo
amemsifu Lowassa kuwa ndiye kiongozi pekee ambaye wakati akiwa Waziri
wa Maji alithubutu kuvunja mkataba mbovu wa kampuni ya City Water
iliyoingia mkataba wa kutoa huduma ya maji jijini Dar es Salaam.
“Unawezaje
kumtukana mtu, sijui eti ni mgonjwa sijui nini. Hana kosa yule mtu.
Amefanya nini, kwa nini kama Lowassa ni mwizi asikamatwe? Viongozi wa
CCM wangapi ni wezi na ambao tayari wameshakamatwa, lakini Lowassa
hakamatwi?” amehoji.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: