![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Polisi katika mji wa Bangalore
kusini mwa India wanamsaka dereva mwenye gari ambalo hutumiwa
kusafirisha pesa za kuwekwa kwenye mitambo ya ATM baada yake kutoweka na
rupee milioni 9.2 ($134,000; £107,000) zikiwa kwa noti mpya za rupee
elfu 2.
Dominic Selvaraj, anadaiwa kutoweka na gari hilo pale mwenzake alipoingia ndani ya choo cha benki kuenda haja.
Polisi wamesema gari hilo lilipatika limeegeshwa mjini Bangalore baadaye siku hiyo.
Mashine za ATM zimeshuhudia milolongo mirefu wa watu tangu noti za
500 na 1000 kupigwa marufuku kama njia ya kukabiliana na ufisadi.
Serikali imezindua noti mpya za rupee 500 na 2,000, lakini bado
hazijaanza kuzunguka vyema kwenye mfumo wa pesa nchini humo na benki
nyingi zinakabiliwa na uhaba wa pesa hizo mpya.
Afisa mkuu wa polisi Charan Reddy amemwambia mwandishi wa BBC Imran
Qureshi kwamba Bw Selvaraj alikuwa ameajiriwa kama dereva wiki tatu
zilizopita na kampuni ya usafirishaji wa pesa kutoka kwenye benki hadi
mitambo ya ATM.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: