![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Muuguzi wa Hospitali
ya Mkoa wa Mbeya anayedaiwa kumkamshifu Junes Elias, mkazi wa Mbozi
mkoani Songwe na Rais John Magufuli ametambuliwa.
Mganga
mkuu wa hospitali hiyo, Dk Gloria Mbwille alisema muuguzi huyo
ametambuliwa na kwamba tume imeundwa kuchunguza tuhuma zinazomkabili.
Hata
hivyo, alikataa kuzungumzia zaidi kuhusu muuguzi huyo wala kumtaja jina
akisema taarifa zaidi zitatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla
baada ya tume kukamilisha uchunguzi huo. Juzi mchana, Junes alimueleza
Makalla kwamba alifika hospitalini hapo Novemba 22 asubuhi akitokea
wilayani Mbozi.
Alisema
baada alifuata taratibu za kufungua kadi kwa gharama ya Sh5,000 kwa
ajili ya kutaka matibabu ya mtoto wake, Joyce Asifiwe (9), lakini
alikashfiwa kwenye dirisha la dawa akiambiwa ataisoma namba kwa
kumchagua Rais Magufuli.
Alisema baada ya kumuona daktari aliandikiwa dawa za kwenda kuchukua kwenye dirisha ambako ndiko alikotolewa maneno ya kashfa.
“Kwenye
dirisha hilo nilimkuta muuguzi mmoja ambaye aliniambia kwamba dawa zote
zinauzwa. Hapa hakuna dawa za bure, si mlimchagua Magufuli, sasa
mtaisoma namba,’’ alisema akidai kumnukuu aliyemtaja kuwa ni muuguzi.
Baada ya
kumsikiliza malalamiko hayo, Makalla aliagiza mganga mkuu aitwe, lakini
ilielezwa alikuwa safarini, hivyo kaimu wake, Dk Ismail Macha alifika.
Makalla
alimueleza Dk Macha kwa kifupi yaliyojiri kutoka kwa mlalamikaji huyo
na kumtaka waongozane hadi hospitalini na kuwaita wauguzi waliokuwa zamu
Novemba 22 dirisha la dawa ili amtambue mhusika na achukuliwe hatua
jambo ambalo limefanyika.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: