Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema wamekubaliana na
Rais wa Zambia Edgar Lungu katika kubadilisha sheria ya kumpata
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli la Tazara ili kusaidia kumpata
mtendaji mwenye weledi.
Jukumu kubwa la Mtendaji huo itakuwa ni kuinua uwezo wa shirika hilo katika kukuza uchumi wa mataifa hayo mawili.
Rais Dkt. Magufuli amebainisha hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam
baada ya kukutana na Rais wa Zambia aliyekuja nchini ambapo amesema
TAZARA haifanyi kazi vizuri kutokana na uongozi ambao umezorotesha
uzalishaji.
Amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 1976 lilipoanzishwa shirika
hilo lilikuwa na uwezo wa kusafirisha tani milioni 5 na sasa imeshuka
hadi kufikia tani 128,000 kutokana na kuwepo kwa matatizo yasiyoisha
yakiwemo migogoro ya wafanyakazi.
Rais Dkt. Magufuli ametaja sehemu ya mazungumzo yao kuwa ni pamoja na
kuendeleza ushirikiano wa bomba la mafuta, ushirikiano katika ukuzaji
wa uchumi, ujenzi wa kituo cha pamoja cha usafirishaji, ushirikiano
ikiwemo kuunganisha kwa gesi ya Ethanol na Uunganishaji wa umeme baina
ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Rais wa Zambia Edgar Lungu amesema wataendeleza
ushirikiano baina ya nchi yake na Tanzania pamoja na kusifu utendaji wa
Rais Dkt. Magufuli katika kuinua uchumi wa nchi na kuendeleza
ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: