Mbunge wa Kigoma
Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amewasilisha rasmi muswada binafsi wa
Sheria ya Mabadiliko ya 15 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kuhusu mafuta na gesi ya Zanzibar.
Zitto
amesema amefanya hivyo katika kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa
Kidemokrasia wa ACT Wazalendo uliofanyika Oktoba 2016, baada ya mjadala
wa mada kuhusu Zanzibar na Katiba ya Muungano.
Zitto alisema hoja hiyo inakuwa muhimu kwa sasa kwa sababu ya kunusuru uvunjwaji wa Katiba ulio wazi.
“Kusubiri
Katiba Mpya hakuhalalishi iliyopo kuvunjwa. Kwa kuwa mabadiliko ya
Katiba Mpya yamekwama bila ya kauli ya Serikali kujua lini mchakato
utaendelea, hii hoja yetu ni ya lazima kwa sasa katika kuhalalisha hatua
ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ya kutunga sheria inayohusiana
na mafuta na gesi asilia,” alisema Zitto.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: