ads

Serikali imesema kuwa kuanzia mwakani nauli zote za mabasi yanayotoa huduma za usafirishaji abiria mijini maarufu kama daladala zitakuwa zinalipwa na abiria kupewa risiti za mashine za kielektroniki


Imesema lengo la mpango huo ni ili kubaini kipato halisi cha wamiliki wa mabasi hayo na kuimarisha ukusanyaji kodi.

Kauli hiyo imetolewa  Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabarani kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Majini na nchi Kavu SUMATRA Bw. Johansen Kahatano wakati wa uzinduzi wa kamapeni ya uvaaji sare kwa madereva daladala nchini.

Amesema kuwa zoezi hilo liko katika hatua za ukamilishaji na kuanzia mwezi wa kwanza mwakani mfumo huo utaanza kutumika lengo likiwa kuboresha na kubadilisha uhusiano baina ya mmiliki na mfanyakazi wa gari.

Amesema malipo hayo yatasaidia serikali kufikia lengo lake la kuifanya ajira ya udereva kuwa rasmi kama kazi nyingine kwa kuwa mapato yote yatakuwa yanaonekana serikalini na kuwabana wamiliki wa magari kutoa ajira za mikataba kwa wafanyakazi wao.

Sambamba na hilo serikali imetoa muda wa wiki mbili kwa wamiliki wa daladala kununua sare za wafanyakazi wao na kwa wale watakaokiuka maagizo hayo watafutiwa leseni zao.

Kwa upande wa madereva kwa kupitia Mwenyekiti wao Bw. Shabani Mdemu amesema wamekubaliana na maagizo hayo kwakuwa lengo lao ni kwamba serikali ihalalishe kazi ya udereva ili wapate haki zao za msingi hasa malipo yao ya msingi.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: