KASI kubwa ya kuzifumania nyavu ambayo
mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga raia wa Zambia, Obrey Chirwa ameanza
kuionyesha hivi karibuni katika michuano ya Ligi Kuu Bara imewafanya
wale waliokuwa wakimpuuza awali kuwa hana lolote kufuta kauli zao na
kuanza kumuombea mema kwa Mungu.
Mmoja kati ya watu hao ni Mzee Ibrahim
Akilimali ambaye siku chache baada ya Chirwa kutua nchini alianza
kumponda kuwa hana lolote na kiwango chake siyo cha kuitumikia timu
hiyo, hivyo Yanga imepoteza fedha zake kwa kumsajili.
Hata hivyo, mzee Akilimali alifuta kauli
zake hizo alizokuwa akizitoa kwa Chirwa baada ya kusema kuwa alikuwa
akifanya hivyo kwa lengo ya kumjenga ili aongeze bidii uwanjani.
Alisema kwa sasa anafurahishwa na
kiwango cha mshambuliaji huyo, kwani hivyo ndivyo alivyokuwa akitaka
afanye kwa faida ya timu ambayo ilimsajili kwa mamilioni ya fedha kuliko
mchezaji mwingine yeyote klabuni hapo.
“Ujue watu walikuwa wananielewa vibaya
lakini lengo langu lilikuwa ni kumfanya aongeze bidii na sikuwa na nia
nyingine dhidi yake.
“Lakini kwa sababu ameanza kufanya kazi
tuliyokuwa tukiikusudia kutoka kwake, sina tena tatizo naye na sasa
namuombea kwa Mungu aendelee kufanya vizuri, kama kulikuwa na watu
wamemfunga miguu basi washindwe,” alisema Akilimali.
Mpaka sasa, Chirwa amefunga mabao matano kwenye mechi nne alizoanza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: