Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe ameanza kuikaba koo Serikali ya Awamu ya Tano
akisema ataifikisha Mahakamani ili chombo hicho cha kusimamia sheria
kitoe tafsiri ya kuhusu vitendo alivyosema ni kwa ukandamizaji wa
demokrasia vinavyofanywa na viongozi wake hasa mkoani Arusha.
Amelaani
kitendo cha mkuu wa Wilaya ya Arumeru kuwasweka ndani madiwani wanne wa
chama hicho akisema hiyo ni ishara ya kwamba utawala wa awamu ya tano
hauheshimu sheria na kwamba amewaagiza wanasheria wake kwenda mahakama
kupata tafsiri kuhusu vitendo hivyo.
Mbowe
amesema viongozi hao wamekuwa wakifanya vitendo vya udhalilishaji kwa
baadhi ya wabunge, madiwani, mameya na wenyeviti wa halmashauri kinyume
na sheria.
“Wakuu
hao wa wilaya pamoja na mkuu wa mkoa wamekuwa wakiwadhalilisha
wawakilishi wa wananchi ilhali wao ni waajiriwa na hawajaomba kura kwa
wananchi,” alisema.
“Nawashangaa
sana wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ambao jambo hili limeanza mwaka
huu, hii ni nafasi mbaya sana kwa Rais Magufuli kuchagua makada badala
ya watumishi,” amesema Mbowe.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: