CHAMA cha ACT Wazalendo kimeazimia kufanya maadhimisho ya miaka 50 ya
Azimio la Arusha Februari mwakani pamoja na kueleza mafanikio na
changamoto zake.
Maazimio hayo yametokana na mkutano wake wa kwanza wa kisera, uliofanyika tangu Uchaguzi Mkuu wa 2015 umalizike.
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Ofisa Habari
wa ACT Wazalendo, Abdallah Khamis, ilieleza kuwa maadhimisho hayo,
yatatanguliwa na Halmashauri Kuu ya chama katika eneo ambalo Chama cha
TANU kilifanya mkutano uliozaa Azimio la Arusha mwaka 1967.
Khamis alisema katika maadhimisho hayo, imeshauriwa wataalamu
mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wawepo kwa ajili ya kujadili
mafanikio na changamoto za Azimio la Arusha katika miaka 25 ya
kutekelezwa kwake na madhara yake tangu lizikwe huko Zanzibar mwaka
1992.
Aidha, ACT imeazimia mchakato wa kuandika Katiba mpya ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, uanze sasa kwa kufanya marekebisho ya sheria ya
kura ya maoni na sheria ya mchakato wa Katiba.
Alisema chama hicho kimemuomba Rais John Magufuli, kuunda timu ya
wataalamu kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba
na kuitisha mkutano mkuu wa kikatiba wa wananchi ili kupitisha katiba
pendekezwa na kwenda kwenye kura za maoni.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: