![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
KIONGOZI Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, amemuunga
mkono Rais John Magufuli, kwa kuwakataza wafuasi wote wa chama hicho,
kutojihusisha na maandamano ya aina yoyote kwa kuwa chama hicho
hakijatangaza maandamano.
Kauli hiyo ya Zitto, imekuja siku moja
baada ya Rais Magufuli kuonya kuwa atakayethubutu kuandamana atakiona
cha mtema kuni, huku Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum
Mwalimu, akitangaza kuwa maandamano ya wafuasi wa chama hicho nchi
nzima, yako pale pale.
Katika taarifa yake aliyotoa jana kwa
vyombo vya habari, Zitto amesisitiza kwa wanachama hao na wafuasi wa
chama hicho, kutojihusisha na maandamano ya aina yoyote kwa kuwa chama
hicho hakijatangaza maandamano.
Katika hatua nyingine Zitto
amewataka wafuasi hao, kutoona aibu kuunga mkono uamuzi wowote wa
serikali au chama chochote cha siasa, unaoendana na azimio la Tabora
hususan katika vita dhidi ya ufisadi na kurejeshwa kwa miiko ya uongozi.
“Tuwe
mstari wa mbele kupinga ufisadi kwani rushwa ni adui wa haki. Tuwe
mstari wa mbele kutaka kurejeshwa kwenye miiko ya uongozi, sisi ndiyo
chama pekee chenye itikadi iliyo wazi, tuisimamie popote tulipo bila
woga wala aibu,” ilieleza taarifa hiyo.
Katika taarifa yake hiyo,
Zitto amewataka wanachama wa chama hicho kusoma, kuelewa na kujadili
Azimio la Tabora na kuchambua muktadha wake katika mazingira ya sasa ya
siasa za nchini, kwa kuwa chama hicho kiliundwa kwa madhumuni ya
kurejesha nchi kwenye misingi yake.
Kuandika barua
Aidha,
ameagiza kila mwanachama wa chama chake aandike barua kwa Rais Magufuli
kwa namna anavyoona yeye kumtaka alichodai kuacha kuingiza nchi kwenye
utawala wa imla.
“Chama chetu kina wanachama 431,120 wenye kadi,
Ikulu ikipata barua 200,000 kutoka kila kona ya nchi itafunguka macho,”
ilidai taarifa hiyo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: