![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
RAIS John Magufuli, ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bagamoyo, Azimina Mbilinyi ambaye amehudumu katika cheo hiko
kwa siku 24 tu.
Taarifa ya Ikulu iliyotumwa jana kwa vyombo vya
habari na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (Tamisemi), Musa Iyombe, imesema kuwa Rais hajaridhishwa na
utendaji wake.
Ingawa taarifa hiyo haikufafanua zaidi, lakini
wakati wakurugenzi hao walipokuwa wakila Kiapo cha Uadilifu wa Uongozi
wa Umma katikati ya mwezi huu, Rais Magufuli alisema kila mkurugenzi
aliyechaguliwa, atambue kuwa sifa zake zilichambuliwa na Rais mwenyewe.
![]() |
Azimina Mbilinyi,aliyekuwa Mkurugenzi Bagamoyo |
Hata
hivyo, aliwataka kuhakikisha wanasimamia vyema fedha za serikali
zinazowasilishwa katika halmashauri na kuepuka kuburuzwa, kujipendekeza,
kukejeliwa au kutumika vibaya kwa kuingia mikataba na kampuni feki
zisizoweza kutekeleza vyema wajibu wake.
Magufuli alisema anazo
taarifa za baadhi ya wakurugenzi, walikuwa wakishirikiana na mameya,
madiwani na wenyeviti wa halmashauri kwa kupitisha na kuingia mikataba
na kampuni zilizo na uwezo chini ya viwango katika kutekeleza miradi ya
barabara na matokeo yake miradi mingi haikuwa na mafanikio.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: