![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Wanachama wa klabu
ya Simba wanakutana katika mkutano mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika
kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam leo.
Licha
ya kuwapo na agenda mbalimbali ikiwamo ya usajili, mapato na matumizi
ya klabu na maendeleo ya klabu, suala kubwa linalotarajia kuibua mvutano
ni uwekezaji wa Mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘MO’ aliyepanga kuwekeza
Sh20bilioni katika klabu hiyo.
Uzoefu
wa klabu za Simba na Yanga, viongozi hubanwa hasa eneo la mapato na
matumizi ya klabu, lakini safari hii linaonekana kutokuwa na nguvu zaidi
ya suala la uwekezaji wa MO klabuni hapo.
Suala
hilo ndilo linalofanya wanachama na mashabiki wa Simba kuzozana kila
mahali huku kila mmoja akitoa hoja kwa kadri ya upeo wake kuhusu
uwekezaji huo.
Baadhi
ya wanachama wa Simba walisema wanatarajia kila hoja itakayowasilishwa
katika mkutano wa leo itapewa uzito unaostahili ili kuhakikisha Simba
inakuwa na umoja na kupata mafanikio.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: