![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
BAADA ya Chadema inayoongoza vyama vinavyounda Ukawa, kuzunguka huku
na huko ikiwemo kususa Bunge na kufanya uchochezi, huku maonyo
mbalimbali yakitolewa, hatimaye Rais John Magufuli, ametoa karipio la
mwisho.
Wiki hii Chadema baada ya kumaliza kikao chake cha Kamati
Kuu, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, ilitangaza kuanza
ilichoita operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta),
itakayofanyika kwa mikutano ya hadhara, itakayotanguliwa na maandamano
nchi nzima, kupinga huo udikteta na utawala kandamizi.
“Wasinijaribu
kwa kulazimisha maandamano siku ya tarehe moja
Septemba...atakayethubutu kufanya hivyo, kitakachompata mmmh, hatasahau
kamwe. Mimi ni tofauti sana, wasije wakanijaribu.
“Sitaki nchi
hii iwe ya vurugu, watakaoleta vurugu mimi nitawashughulikia kikamilifu
bila huruma ...kama wapo watu wanaowatumia wakawaeleze vizuri, mimi
sijaribiwi na wala sitajaribiwa. Wananchi hawa wana shida na siasa nzuri
ni wananchi washibe, siasa nzuri ni wananchi wetu wapate dawa,” ameonya
Rais Magufuli.
Onyo la mwisho
Katika onyo la mwisho
alilotoa Rais Magufuli jana, alianza kwa kufafanua kwamba hajapiga
marufuku wanasiasa kufanya mikutano ya kuhimiza maendeleo kwenye maeneo
yao.
“Kama wewe ni Mbunge wa Jimbo la Hai (kwa sasa Freeman
Mbowe), zunguka kwenye jimbo lako hadi uchoke, si unaacha kwako unaenda
Shinyanga kushawishi watu waandamane. Mimi sijazuia shughuli za
waliochaguliwa kwenye maeneo yao, bali nimekataa mtu kuondoka jimboni
kwake na kwenda kufanya fujo mahali pengine,” alionya.
Ukaidi wa Chadema
Katika
kudhihirisha ukaidi wao, Chadema jana iliitisha mkutano na vyombo vya
habari, ambapo katika muendelezo wa siasa hizo, Naibu Katibu Mkuu wake
Zanzibar, Salum Mwalimu, alisisitiza kuwa azma yao ya kufanya mikutano
yake ya hadhara nchi nzima, kuanzia Septemba mosi mwaka huu iko pale
pale.
“Tumewaita hapa kwanza kusisitiza azma yetu ya Septemba mosi
kuwa ni siku ya kukataa udikteta, utawala kandamizi na ukandamizaji iko
pale pale, hatutarudi nyuma, hatutishiki na hatutetereki,” alisema
Mwalimu.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: