![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
WAKATI suala la serikali kuhamia mkoani Dodoma likiwa dhahiri zaidi
kila siku moja inayoongezeka, Rais John Magufuli ametangaza kuuza
majengo ya wizara Dar es Salaam, mara atakapohamia yeye katika makao
makuu hayo ya nchi.
Akizungumza jana kwenye mkutano wa hadhara mkoani Singida, katika
siku ya kwanza ya ziara yake itakayomfikisha mikoa minne, Rais Magufuli
alisema atahakikisha anauza baadhi ya majengo hayo kwa mnada, ili wale
wasiotaka kuhama, wahame kwa lazima. Mbali na Singida, mikoa mingine
atakayotembelea katika ziara hiyo aliyoanza jana ni Tabora, Shinyanga na
Geita, ambako atazungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.
Katika mikutano hiyo, Rais Magufuli anatarajiwa kushukuru wananchi
kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, na kueleza juhudi
zinazofanywa na serikali kutatua kero zao na kuwaletea maendeleo.
Majengo mazuri Katika tangazo hilo, Rais Magufuli amesema majengo
atakayoanza nayo, ni yale yanayotazama bahari; ambayo ndiyo mazuri
zaidi, yenye mwonekano mzuri kutoka ofisini.
“Atakayeng’ang’ania kubaki huko, ajue hana kazi wala mshahara.
Hatuwezi kuendelea kukaa miaka hamsini tunaimba tu kuhamia Dodoma,
wakati hatutekelezi uamuzi wetu hadi wengine wameshatangulia mbele za
haki,” alisema.
Alisema anajua akiitisha zabuni ya ofisi hizo, wateja watayakimbilia
kwa wingi, hivyo wataong’ang’ania kubaki Dar es Salaaam, watakuwa
wamejifukuzisha kazi wenyewe.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: