![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru), imeanza kuchunguza kashfa ya Sh. bilioni 60 inayolikabili
Jeshi la Polisi baada ya kuibuliwa na Rais John Magufuli hivi karibuni.
Rais Magufuli aliibua kashfa hiyo wakati akiwaapisha Naibu Makamishna
wa Polisi (DCP) na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi (SACP)
baada ya kuwapandisha vyeo na kula kiapo cha uadilifu wa utumishi wa
umma, Julai 18, mwaka huu Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Kuhusu kashfa hiyo, Rais Magufuli alieleza kuwa mwishoni mwa mwaka
jana kuna mtu ndani ya Jeshi la Polisi alipewa kazi ya kununua sare za
Jeshi la Polisi na kupewa fedha lakini hakutimiza wajibu huo hadi mwaka
huu.
“Naomba suala hili lifuatiliwe, wapo wanaosema fedha zilizotolewa
zilikuwa Sh. bilioni 20, wengine Sh. bilioni 60, kwa hiyo Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Projest Rwegasira wewe ni
mwanasheria, waliohusika wapelekwe mbele ya haki,” alisema Rais
Magufuli.
Akizungumza na Nipashe jana kwa simu, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru,
Kamishna Valentino Mlowola, alisema suala hilo walianza kulifanyia kazi
tangu walipopata taarifa.
Alisema hadi sasa uchunguzi unaendelea kuhusu suala hilo kwani tuhuma
zozote zenye viashiria vya rushwa zinapotokea hufanyiwa kazi mara moja
na taasisi hiyo.
“Zoezi hili tulilianza siku ileile aliyosema Rais, uchunguzi
unaendelea kuhusu suala hilo, na uchunguzi wowote utakaousikia wewe uwe
wa kiuchumi, kijamii au kisiasa sisi tunaufanyia kazi,” alisema Mlowola.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: