![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amefanya ziara ya
kushtukiza katika Mgodi wa Dhahabu wa Nyamahuna mkoani Geita na kukuta
Wachina 72 kati ya 100 wakiishi na kufanya kazi bila vibali.
Akizungumza katika mgodi huo unaomilikiwa na Mtanzania, Andrew Obole,
Mwigulu alisema alifika hapo kutokana na kuona taarifa zilizozagaa
kwenye mitandao ya jamii.
Mwigulu alisema taarifa hizo zilimuonyesha Masanja Shokera
akicharazwa bakora na raia wa mmoja wa China, Lee Swii, kwa madai ya
kuiba mawe ya dhahabu Julai 6, mwaka huu.
“Nimefika kuthibitisha nilichokisikia kwamba kuna raia wa kigeni
wanachapa watu hapa. Nimemuona mtuhumiwa wa udhalilishaji na kushangazwa
na kukuta wafanyakazi wa China hapa wapatao 100 kwenye mgodi huo,”
alisema.
Alisema taarifa alizonazo ambazo zipo uhamiaji zinaonyesha kuwa raia
wa China waliopo mgodini hapo ni 28 ambao wana vibali halali vya kuishi
nchini.
Waziri alisema kwa sababu hiyo, aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama
ya Mkoa wa Geita kuwaweka chini ya ulinzi Wachina wengine 72, walinzi
saba na Kaimu Meneja Uzalishaji, Richard Joachim.
“Wakati hawa wakiwa chini ya ulinzi naiagiza Kamati ya Ulinzi na
Usalama Mkoa wa Geita kuchunguza uhalali wa raia hao wa China kuishi
nchini bila ya kuwa na vibali.
Vilevile huyo anayeitwa Lee ambaye anatuhumiwa kumdhalilisha
Mtanzania mwenzetu awekwe chini ya ulinzi na walinzi saba na kumpiga na
kumjeruhi,”alisema.
Masanja Shokera ambaye anayedaiwa kudhalilishwa, , alisema siku
hiyo alivamiwa na walinzi wa mgodi huo akituhumiwa kuiba mawe ya
dhahabu.
Alisema walimpiga na kumfunga mikono na miguu na kuendelea kumwadhibu hali iliyosababisha apoteze fahamu.
“Walionipiga wote nawatambua, ni hawa walinzi wa Kimasai wote
walinishambulia na huyu Mchina alikuja pia kunipiga wakati nimefungwa
kamba… alianza huyu mkuu wa ulinzi, Sitta Dotto kuwaamrisha nikaguliwa
kunipiga kichwani,” alisema.
Mkurugenzi wa mgodi huo, Andrew Obole alisema anachotambua Wachina
waliopo kwake ni 28 na kwamba hao wengine alikuwa hawatambui.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: