![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
WAKATI wadau wa soka nchini wameitaka Yanga
kujipanga upya baada ya nafasi yao ya kusonga mbele katika mashindano ya
Kombe la Shirikisho Afrika kuwa finyu, aliyekuwa Rais wa Simba,Ismail Aden Rage ameishauri klabu hiyo kujiuliza pale ilipokosea ili mwakani waweze kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.
Kauli hizo za wadau zimetolewa jana kufuatia Yanga kukubali kichapo
cha mabao 3-1 kutoka kwa Medeama ya Ghana katika mechi yake ya nne ya
Kundi A iliyofanyika juzi mjini Sekondi- Takoradi.
Rage alisema kuwa Yanga inatakiwa
kukubaliana na matokeo hayo na kuyafanyia kazi makosa yaliyojitokeza
mwaka huu kutojirudia katika msimu ujao.
"Yanga wanatakiwa wajiulize ni kwanini wanafanya vizuri kwenye ligi
ya ndani na mechi za kimataifa wanashindwa, je wanajiandaa zaidi na Ligi
Kuu na kutofanya kipaumbele maandalizi ya mechi za kimataifa hadi
inapelekea kufanya vibaya," alihoji Rage.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: