![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Hatimaye Kada maarufu wa Chadema na aliyekuwa Mgombea Urais wa UKAWA
katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,Mhe Edward Lowassa leo hii ameamua
kuvunja ukimya juu ya ukaribu wake na rafiki yake wa kipindi kirefu Dr
Jakaya Kikwete.
Lowassa ambaye leo alifanya mahojiano na kituo
kimoja cha Luninga,amesema kuwa baada ya tukio la kukatwa kwake wakati
anawania nafasi ya Urais kupitia CCM,kisha kujiunga na Chadema hakupata
nafasi ya kukutana na JK.
Itakumbukwa kuwa JK aliongoza kamati kuu ya Chadema kumkata Lowassa katika mkutano Mkuu wa CCM dodoma Mwaka jana.
Lowassa amesema kuwa hawezi kumuhukumu JK kwa tukio lile zaidi ya kumuachia mwenyewe ajihukumu.
Aidha
katika hatua nyingine Lowassa amesema kuwa anampongeza Rais wa sasa Dr
John Magufuli kwa kuanza vema,ila akadai kuwa kama angekuwa yeye
angeweza kufanya vema zaidi ya Dr JPM.
Amesema kuwa JPM ameanza na
suala la madawati lakini yeye angeanza na suala la kuboresha maslahi ya
walimu kwanza ili kuinua kiwango cha Elimu.
Aidha amependekeza kuwa ni vema Rais Magufuli akawa anashauriwa ili kusudi kuhakikisha anaongoza vema,ikiwemo kuachana na tabia ya kuongoza nchi kwa imla.
Katika
hatua nyingine Lowassa amesema kuwa anamshauri Rias Shein kutafuta njia
muafaka ya maridhiano na CUF ili kuhakikisha usalama wa visiwa hivyo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: