![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Mfanyabiashara
Mohammed Dewji maarufu kama Mo, ametawala katika mkutano wa wanachama
wa Simaba uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Wanachama
walionekana wazi kuwa wana hamu ya kuusikia uongozi wao unasema nini
kuhusiana na kuingia kwenye kampuni ambako Simba itaweza kuuza hisa.
Uamuzi
huo, ulisababisha wanachama kutotaka kujadili chochote zaidi ya kuona
kama uongozi uko tayari kuuza hisa zake asilimia 51 kwa Sh bilioni 20
kwa Mo.
Wakati
wa kujadili ajenda nyingine za kikao kama zile za Hesabu, Chombo cha
uchaguzi na kadhalika, hazikuwa na mvuto na wengi walitaka ajenda namba
tisa ambayo ilikuwa ni “Taarifa ya kamati ya maboresho ya mfumo wa
uendeshaji”.
Lakini
wanachama hao walianza kulalamika wakiona kama uongozi ulipita haraka
hapo. Wakaanza kupiga kelele wakitaka kusikia mjadala.
Mwisho,
Rais wa Simba Evans Avena alilazimika kurejea na kuwaeleza kwamba kama
wanataka Simba kuingia kwenye mchakato wa kampuni, maoni yao
yamesikilizwa na yanaanza kufanyiwa kazi.
Kauli hiyo ya Aveva, ilifanya wanachama hao washangilie kwa nguvu hata yeye baada ya kuufunga mkutano huo.
credit-salehjembe
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: