ads

KOCHA Mkuu wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Yanga Mdachi Hans van der Pluijm amesema kuwa kufanya vibaya kwa timu yake katika michezo minne ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kumetokana na kikosi hicho kutokuwa na bahati kwenye michuano hiyo.


Akizungumza  jana, Pluijm alisema kuwa alikiandaa vizuri kikosi chake kwa ajili ya kusaka ushindi lakini jambo hilo lilishindikana na hatimaye imeambulia pointi moja katika mechi nne za Kundi A ambazo wamecheza.

Pluijm alisema kuwa hata hivyo hajakata tamaa na wataendelea na maandalizi kwa ajili ya kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mechi mbili zilizobakia kwa sababu anaamini kwenye soka lolote linaweza kutokea.

"Hatuko katika nafasi nzuri, tunachotakiwa kukifanya sasa ni kuhakikisha tunatoka hapa, tutajipanga kuhakikisha tunafanya kila linalowezekana ili kufufua matumaini," alisema Pluijm.

Mdachi huyo alisema kuwa kikosi chake kilikuwa na makosa kadhaa ambayo wapinzani wao waliyatumia kupata ushindi tofauti na inavyokuwa kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.

"Wanafanya makosa ambayo katika mechi za Ligi Kuu hawafungwi, lakini katika mashindano haya ya kimataifa, timu zina uzoefu na kutumia nafasi hiyo kupata mabao, ni changamoto mpya ambayo tumekutana nayo kwenye michuano hii, tumejifunza na tutabadilika kwenye mechi zinazofuata," Pluijm alisema.

Aliongeza kuwa mbali na ushiriki wa michuano hiyo ya kimataifa, Yanga pia inajipanga kuikabili Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Hisani unaotarajiwa kufanyika Agosti 17 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Kikosi cha Yanga ambacho kimesharejea nchini kikitokea Ghana, kitaanza mazoezi Jumatatu kwa ajili ya kuikaribisha Mo Bejaia ya Algeria wakati mchezo mwingine wa Kundi A utakuwa ni kati ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dhidi ya Medeama utakaochezwa Ghana.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI


ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: