![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani),
amewaonya wananchi wanaotaka kuvamia njia, litakapopita bomba la mafuta
kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika bandari ya Tanga, kwa kujenga
nyumba ili kulipwa fidia mradi utakapoanza.
Aliwaeleza kuwa bomba hilo lililopewa jina la East Africa Crude Oil
Pipeline, watakaovamia wanapoteza fedha zao na itakula kwao, kwani
watatumia ramani ya satelaiti iliyopigwa Juni mwaka jana, muda ambao
mazungumzo ya ujenzi wa bomba hilo yalianza.
Akizungumza katika mkutano wa makatibu wakuu wa wizara zote pamoja na
wakuu wa mikoa ambao bomba hilo linapita, Muhongo alieleza kuwa watu
hao hawawezi kudanganya kwa lengo la kupata fedha wakidai kuwa bomba
limewakuta.
Alisema kuna satelaiti 1007 zinazofanya utafiti duniani na mpaka
Agosti mwaka jana, zilikuwa zote zikifanya kazi hivyo kuonesha ni
majengo gani yalikuwepo katika njia hiyo, hivyo kutaka wananchi wapewe
ramani inayoonesha bomba litakapopita ili kuepusha gharama.
Muhongo alisema leo atakutana na waziri wa Nishati wa Kongo kwa lengo
la kujadiliana jinsi nchi hiyo itakavyoshirikishwa kwenye mradi huo
mapema, huku akitarajia nchi ya Burundi kuungana katika mradi huo.
Alisema hatua hiyo itawezesha bomba hilo kutumiwa na nchi hizo kupitisha mafuta.
Burundi na Tanzania zinaendelea na utafiti katika ziwa Tanganyika na
yakipatikana watatumia bomba hilo. Muhongo alisema pia wanatarajia
kutumia bomba hilo kusafirisha mafuta kutoka Sudani kusini kutokana na
kuwa ni rahisi kuyasafirisha mpaka Uganda na kutumia bomba hilo.
Bomba hilo la mafuta linatara kutumia Dola za Marekani bilioni 3.5
mpaka litakapokamilika na kutaka katibu mkuu kuunda kamati maalumu ya
kudumu ambayo itakuwa na wajumbe wawili au watatu kutoka kila wizara
kuhakikisha mradi huo unakamilika.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: