ads

Msanii na mwanamitindo Jokate Mwegelo amefunguka na kumwaga sifa za kutosha kwa msanii Alikiba na kusema kuwa ni msanii huyo ni mfalme ila hana mbwembwe kama wasanii wengine.


Jokate alitumia ukurasa wake wa Instagram kumwaga sifa hizo na kudai kuwa akiwa amenuna akisikia sauti ya Alikiba anajikuta anafurahi kwani anavutiwa sana na sauti hiyo.

"Alikiba ni King wa kutoa ngoma baada ya ngoma, King asiye kuwa na mbwembwe, ni mzuri kuliko wote, ni mfalme wa sauti ya kumtoa nyoka pangoni. 

Nikinuna najikuta nafurahi nikisikia sauti yake, hapa nimesikiliza 'Nisamehe' nairudia tu, Nisamehe ni wimbo wa taifa unakuja kwa kasi ya ajabu". Aliandika Jokate 

Alikiba na Baraka the Prince wanategemea kuachia wimbo ambao utaiwa 'Nisamehe' ni wimbo wa Baraka the Prince ameshirikisha Alikiba.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: