ads

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakina mpango wa kumjibu Jaji Francis Mutungi msajili wa vyama vya siasa nchini wala Christopher Olesendeka.


Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema Mutungi amejiondolea sifa ya kuwa mlezi wa vyama vya siasa, sababu ameonyesha upande.

Aidha kuhusu Christopher Ole Sendeka, Mwalimu amesema hana cheo, hivyo akijitokeza mwenye cheo Chadema watamjibu.


“Baada ya Dk John Magufuli, mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kukabidhiwa alisema sekretarieti yote irudi madarakani, cheo cha msemaji wa chama hakipo katika katiba ya CCM sisi hatuwezi kujibizana naye” alisema Mwalimu.

Kwa upande wake, Prof Mwesiga Baregu Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho amesema licha ya kuwa hawakuwa na mpango wa kujibu Mtungi, ameangalia tamko La Chadema hakuna popote kama kulikuwa na kauli za uchochezi.

Uchochezi ni suala kubwa, unapotaja lazima uwe umfanya utafiti na umejiridhisha sio kutamka tu. Jaji Mutungi huyu ni kijana wangu, tamko lake lina mapungufu mengi. Alisema.

Katika hatua nyingine, Chadema imesema itampelekea Mutungi tamko lenye maazimio ya kamati kuu kuhusu mikutano na operesheni Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta).

Inaelekea tamko hilo alilitoa baada ya kusikia au kusoma kwenye vyombo vya habari, kwa hiyo leo tutampelekea kiofisi kabisa ili aonyeshe yalipo matusi na uchochezi aliokuwa anasema.

Hata hivyo chama hicho kimemlaumu Mutungi na kusema ameona tamko la Chadema tu lakini wakati mikutano inazuiliwa na viongozi wa CCM hakusikika akikemea.

“Kuna mateso yanaendelea Pemba watu kubambikizwa kesi, mikutano inazuiliwa nchi nzima, wabunge wetu kule Karatu wamekamatwa kuzuilikuwa kufanya mikutano, tulitegemea hayo ayasemee, lakini yupo kimya, amejiondolea sifa ya kuwa mlezi wa vyama vya siasa sababu ameegemea kusaidia CCM”. Alisema Mwalimu.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: