![ads](http://1.bp.blogspot.com/-J5aEnGVep5k/WJTrf2fzuPI/AAAAAAAAU5U/_iuE-DY1RHAM5_hqPHb-UuNbabG2xn2nwCK4B/s1600/AdvertiseHere.jpg)
Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa mjini (Chadema) amemshauri Dk John
Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuuza kwanza Ikulu
kabla ya kuuza majengo mengine ya serikali ili zipatikane hela za
kuhamia Dodoma,
Msigwa amesema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook na kusisitiza kuwa haamini kama watanzania ni kama ng’ombe wataswagwa swagwa tu.
“We have a serious challenge as a National(tunachangamoto hasa kama taifa), nimshauri Rais aanze kwanza kuuza Ikulu ndipo majengo mengine ya umaa yafuate, nadhani ikulu itapata wateja mapema , tutapata hela za kuhamia Dodoma.” Ilisomeka kauli ya Msigwa.
Mbunge huyo pia amesema haamini kuwa watanzania nikama ng’ombe ambao wataswagwa swagwa tu wakae kimya, na kuonya kuwa mengi watayaona ambayo bado hayajajiri.
Kauli ya Msigwa inakuja ikiwa ni wiki tu tangu serikali ya Magufuli kutangaza mpango wake wa kuhamishia serikali yote mkoani Dodoma kabla ya mwaka 2020.
Magufuli alitoa kauli hiyo, wakati akihutubia mkutano mkuu maalum wa chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM) – tarehe 23 Julai. Mkutano mkuu wa CCM uliomalizika mkoani Dodoma wiki iliyopita, ulimchagua Dk. Magufuli, kuwa mwenyekiti wa tano wa chama hicho.
Katika hotuba yake mbele ya wajumbe, Magufuli ameeleza kile alichoita, “dhamira yake ya dhati ya kukamilisha mpango wa serikali wa kuhamia Dodoma.”
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: