Tanzania, Zambia pamoja na Jamhuri ya watu wa China zimeanza
mazungumzo ya pamoja kwa lengo la kushirikiana kuimarisha sekta ya
miundombinu hususan kufufua Reli inayounganisha Tanzania na Zambia
(TAZARA) ili kukuza biashara na uwekezaji.
Akizungumza katika mkutano huo katibu mkuu kiongozi balozi John
Kijazi, amesema lengo ni kuangalia changamoto zilizopo, ikiwemo za
kisheria na kiutawala katika shirika hilo ili hatimaye liweze kufanya
kazi kwa namna iliyokusudiwa.
Awali reli hiyo iliweza kusafirisha tani zaidi ya milioni 2 za bidhaa
kwa mwaka, wakati sasa inasafirisha tani laki 2 kwa safari inayotumia
hadi siku kumi na mbili kutoka Dar es saalam hadi New Kapiri Mposhi
wakati malori yanatumia siku tano pekee.
Balozi Kijazi amesema lengo ni kuifufua Reli ya TAZARA ambayo ni
kiungo muhimu na alama kubwa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia,
kwa kuangalia umuhimu wa reli hiyo ni wa kihistoria ambao unahusisha
nchi tatu za Tanzania, Zambia na Jamhuri ya Watu wa China ambao kwa
kiasi kikubwa walichangia ujenzi wa reli hiyo.
Awali Tanzania na Zambia zilikubaliana kuwekeza zaidi katika reli
hiyo ikiwemo kuboresha uendeshaji na ukarabati ili kuirejesha katika
hali yake ya awali na hatimaye kukuza biashara na uwekezaji.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: