Kocha wa Simba, Jackson Mayanja, ameanza kuweka hadharani mipango ya
kukisuka upya kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao wa 2016-17 ambao
unatarajiwa kuanza mwezi August.
Mayanja ambaye alikabidhiwa kikosi cha Simba mwanzoni mwa mwaka huu,
baada ya kuondolewa kwa kocha kutoka nchini England Dylan Kerr,
amesisitiza kutengeneza kikosi kilichosheheni wachezaji wenye uzoefu wa
kupambana.
Kocha huyo kutoka nchini Uganda, amesema anaamini wachezaji wenye
kaliba ya uzoefu na ushindani ndio watakua jibu la klabu hiyo kongwe,
kuondokana na matatizo ya kufanya vibaya hadi kufikia hatua ya kushindwa
kutwaa ubingwa kwa mwaka wanne mfululizo sasa.
Simba ambayo mpaka sasa imeshapoteza matumaini ya kutwaa taji lolote,
msimu huu ukimalizika watakuwa wanatimiza mwaka wa nne mfululizo bila
ya taji la Ligi Kuu Bara huku msimu wao wa mwisho kubeba taji hilo ukiwa
ni wa 2011/12.
Mayanja amesema wachezaji wazoefu ndiyo wanapaswa kusajiliwa na Simba
katika kipindi kijacho cha usajili ili msimu ukianza waweze kuendana na
kasi ya ligi.
“Simba inatakiwa kusajili wachezaji wengi wazoefu waliokomaa tayari
na wanajua kuwa soka ndiyo kazi yao kama ilivyo kwa Yanga na Azam.
“Hali hiyo itatusaidia sana kuendana na kasi ya ligi na itatusaidia
kutimiza malengo yetu ambayo tunahitaji kuyatimiza ikiwa ni pamoja na
kutwaa mataji mengi,” alisema Mayanja.
Hata hivyo haifahamiki kama Mayanja ataendelea kuwepo Msimbazi kwa
kipindi kingine, kutokana na uongozi wa klabu hiyo kukaa kimya mpaka
sasa juu ya mustakabali wa kocha huyo ambaye aliwahi kuzinoa Kagera
Sugar pamoja na Coastal Union.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: