Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli
ameiagiza mifuko ya hifadhi za jamii nchini kubadilisha aina ya
uwekezaji badala ya kuendelea kuwekeza katika majengo badala yake waanze
kuwekeza katika ujenzi wa viwanda
Rais amesema ni vyema viongozi na wataalamu waliopo katika mifuko ya
hifadhi nchini kuanza kufikiria nje ya ukuta kwa kuanza kujenga viwanda
ambavyo vitakuwa na manufaa makubwa kwa watanzania wengi hasa vijana
ambao watapata ajira katika viwanda hivyo.
Amesema tofauti na ilivyo sasa pamoja na uwekezaji huo watu wachache
wenye kipato kikubwa ndio wamekuwa wakimudu kukodi majengo hayo huku
watanzania wengi masikini wakishindwa kumudu gharama za pango hivyo
kufanya majengo hayo kukosa wapangaji.
Awali wakizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo la PPF mjini
Arusha lenye ghorofa 8 lililogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 33.91
waziri wa fedha Dakta Philip Mpango na waziri wa sera,bunge,kazi,ajira
na watu wenye ulemavu Jenisther Mhagama wamewapongeza PPF kwa uwekezaji
huo na kusema kuwa hakuna taifa lolote linaloweza kuendelea bila
uwekezaji wa ndani na nje.
Nae mkurugenzi mkuu wa PPF William Erio amesema kuanzia mwaka wa
fedha 2016/2017 mfuko umeanza mkakati wa miaka mitatu wa kutekeleza
agizo la rais magufuli la kuwekeza katika viwanda vitakavyotumia
malighafi inayopatikana hapa nchini.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: