ads

Wanawake wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamesema kuwa licha ya kesho kurejea katika vikao vya bunge baada ya kususia ila msimamo wao wa kujiondoa katika umoja wabunge wanawake upo pale pale.

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Halima Mdee, amesema kuwa tayari wameshaandika barua kwa Naibu Spika kuhusiana na suala hilo na wanasubiri maamuzi yake.

Mhe. Halima Mdee amesema kuwa wameamua kufanya hivyo baada ya kuona umoja huo ambao ulitakiwa kukemea matendo ya udhalilisha kwa wabunge wanawake haujalipa uzito wa suala hilo ambalo limeelekezwa kwa wabunge wanawake wa vyama vya upinzani.

Mhe. Mdee amesema kuwa hatima yao ya kurudi katika umoja hou wa wabunge wanawake itategemea na Naibu Spika ambae pia ni kiongozi katika umoja atajibu nini na baada ya hapo watakaa kujadili ni jinsi gani wataweza kushirika katika umoja huo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: