KIUNGO wa Zimbabwe anayechezea Simba, Justice Majabvi, amesema yupo
tayari kubaki kuendelea kuichezea timu hiyo msimu ujao kama atapewa ofa
ya kuridhisha.
Mkataba wa kiungo huyo unamalizika baada ya ligi kumalizika mwezi huu
na hadi sasa amesema hajaanza mazungumzo ya kuongeza mkataba.
, Majabvi, alisema angependa kubaki
kuichezea timu hiyo kutokana na kazi nzuri na ushirikiano kutoka kwa
viongozi na wachezaji wenzake, lakini itakuwa ngumu kama hatopewa
mkataba mpya.
“Siwezi kulazimisha kupewa mkataba kwa sababu benchi la ufundi na
hata viongozi wanaujua uwezo na mchango wangu niliotoa kwa Simba, kwa
hiyo maamuzi wanayo wao, ingawa binafsi ningependa kubaki Simba ili
niendeleze jitihada zangu za kuipa timu mafanikio,” alisema Majabvi.
Kiungo huyo alisema yapo mambo mengi yamemvutia kwenye ligi ya
Tanzania, moja ikiwa ni upinzani uliopo baina ya Simba na Yanga, ambao
hajawahi kuuona katika nchi nyingi alizocheza.
Pia alisema amekuwa akipata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu
hiyo, kiasi cha kujisikia kama yupo kwao Zimbabwe, ispokuwa kitendo cha
kushindwa kupata mafanikio ndiyo kimemuumiza.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: