ads



Klabu ya Yanga ya Tanzania imepangwa kukutana na klabu ya Sagrada Esperanca Angola katika hatua ya mtoano (16 bora) ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.


Yanga itaanzia nyumbani kati ya tarehe 6 hadi 8 mwezi Mei, na marudiano itakuwa nchini Angola kati ya tarehe 17 na 18 mwezi huohuo.

Yanga imefikia hatua hiyo baada ya kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Mabingwa Barani Afrika na Al Ahly baada ya kufungwa 2-1 katika mchezo wa marudiano uliopigwa jana nchini Misri.

Jumla ya timu 8 zilizotolewa katika michuano hiyo pamoja na Yanga zimeshushwa katika michuano ya Kombe la Shirikisho na kukutana na timu nyingine 8 zilizofuzu kutoka raundi ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho.

Shirikisho la Soka Barani Afrika limeendesha droo muda mfupi uliopita na matokeo ya droo hiyo ni kama ifuatavyo.

MO Bejaia (Algeria) vs Esperance (Tunisia)

Stade Malien (Mali) vs FUS Rabat (Morocco)

Etoile du Sahel (Tunisia) vs CF Mounana (Gabon)

TP Mazembe (DR Congo) vs Stade Gabesien (Tunisia)

Ahli Tripoli (Libya) vs Misr Makassa (Egypt)

El Merreikh (Sudan) vs Kawkab (Morocco)

Young Africans (Tanzania) vs Sagrada Esperanca (Angola)

Mamelodi Sundowns (South Africa) vs Medeama (Ghana)

Michezo yote ya kwanza itachezwa kati ya tarehe 6 na 8 mwezi Mei na marudiano ni kati ya tarehe 17 na 18 mwezi Mei.

Kati ya timu hizo 16, timu nane zilizofuzu 8 bora kupitia michuano hiyo ni Esperance (Tunisia), Stade Gabesien (Tunisia), FUS Rabat (Morocco), Misr Makkassa (Egypt), Esperanca (Angola), CF Mounana (Gabon), Kawkab (Morocco) wakati Medeama (Ghana).

Timu zilizofikia hatua hiyo kutokana na kutolewa katika michuano ya Mabingwa Afrika ni TP Mazembe (DR Congo), Etoile du Sahel (Tunisia), El Merreikh (Sudan), Stade Malien (Mali), MO Bejaia (Algeria), Ahli Tripoli (Libya), Mamelodi Sundowns (South Africa) na Young Africans (Tanzania)

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: