Katika mjadala wa leo bungeni, mbunge wa CHADEMA viti maalum kutoka mkoa
wa Geita, Upendo Peneza amlipua Rais Magufuli ya kwamba anapaswa
kuonyesha mfano katika kulipa kodi kutoka kwenye mshahara wake ambao kwa
sasa haukatwi kodi..
Hali hiyo ilizua taharuki ambapo waziri wa ofisi ya Rais, TAMISEMI Simbachawene aliinuka na kuomba kutoa taarifa. Katika kutoa kwake taarifa waziri alisema mshahara wa Rais haujadiliwi popote pale, ikiwa ni sharti ndani ya katiba ibara ya 43.
Mbunge Peneza katika kukataa taarifa hiyo alisema hoja yake ya msingi ni kutaka Rais aonyeshe kuongoza kwa mfano kwa kulipa kodi kama anavyosisitiza wananchi na wafanyabiashara kulipa kodi.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: