BAADA ya kutoka kwenye michuano ya kimataifa, Yanga na Azam leo
zinageukia Kombe la Shirikisho la TFF (FA) zikiwania kucheza
fainali,Yanga itakuwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga kumenyana na
Coastal Union katika mechi ya nusu fainali ya michuano hiyo ya FA.Mechi
hiyo inatarajiwa kuwa ngumu kwa pande zote hasa kutokana na matokeo ya
karibuni ya timu zote mbili.
Coastal iliyo mkiani mwa msimamo wa
Ligi Kuu inaonekana kuzinduka baada ya kuiondoa Simba kwenye robo
fainali za michuano hiyo, lakini pia ikishinda mechi zake zilizosalia za
Ligi Kuu.
Yanga iko vizuri baada ya ku toka Misri kucheza na Ahly
na kuonesha kiwango cha juu, hakuna shaka kwamba leo inapewa nafasi
kubwa ya kuibuka na ushindi, licha ya kwamba Yanga ilipoteza mechi ya
Ligi Kuu dhidi ya Coastal kwenye uwanja huo.
Kocha wa Yanga, Hans
van der Pluijm amesema Coastal Union isitarajie ushindi katika mchezo wa
leo kwani hata yeye timu yake inalitaka kombe hilo..
“Coastal
wasitarajie kuifunga tena Yanga kama ilivyokuwa kwenye mechi ya ligi
tunakwenda tukiwa na mfumo mpya ambao tumeanza kuutumia kwenye mechi
mbili zilizopita dhidi ya Mtibwa Sugar na Al Ahly, nadhani huu utakuwa
muafaka kwao kuhakikisha tunashinda na kutinga fainali,” alisema Pluijm.
Kwa
upande wa Azam, itakuwa Mwadui kumenyana na Mwadui ya Shinyanga mechi
ambayo kocha wa timu hiyo Stewart Hall amesema ni muhimu kwao kushinda.
“Mazingira
yanatulazimisha kushinda mechi ya kesho (leo), tumetolewa kwenye
mashindano ya Afrika, tunashika nafasi ya tatu kwenye mbio za ubingwa
hivyo ili matumaini ya kushiriki kimataifa mwakani yawe makubwa ni
lazima tuifunge Mwadui,” alisema.
Akiizungumzia mechi hiyo kocha
wa Mwadui, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ alisema amejipanga kuitoa Azam na
kwamba timu yake ndio bingwa wa michuano hiyo,Mwadui ilitinga nusu
fainali ya kombe hilo baada ya kuifunga Geita mabao 3-0 katika mchezo
uliochezwa Shinyanga.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: