Msanii wa Bongo Flava Mr. Blue amesema kuoa siyo kigezo cha kushuka
katika utendaji wa mwanamuziki na maisha kwa ujumla kama inavyodhaniwa
na watu wengi.
Msanii
huyo ameyasema hayo katika kipindi cha eNEWS kinachorushwa na kituo cha
Eatv ambapo mtangazaji alimuuliza kuhusiana na yeye kuoa na haoni
kwamba anaweza kushuka katika kazi zake za sanaa.
Mimi siwezi kufeli kwenye muziki nimepata mitihani mingi kwenye muziki lakini sjashuka hadi leo, nimeanza muziki nikiwa mtoto na sasa hivi nimeshapata mtoto bado nipo kwenye muziki.
''Muziki ni kazi wapo wasanii wengi wa Marekani wameoa lakini wanafanya vizuri , kwa Tanzania mfano Mzee Yusuf ameoa mara mbili lakini sio kwamba ameshuka kwenye game kwa hiyo habari hizi siyo za kweli kabisa''- Amesisitiza Mr. Blue.
Mr. Blue amefunga ndoa hivi karibuni jijini Dar es salaam ambapo kwa sasa ana wawili.

DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: